JENGA AFYA NA TOKOMEZA UMASIKINI KUTUMIA KAMPUNI YA KITANZANIA.


JATU PUBLIC LIMITED COMPANY UFAFANUZI
~ last updated
JATU PLC ni kampuni ya UMMA ambayo imejikita katika Kilimo, Viwanda, Masoko na Mikopo.
USAJILI NA UHALALI
kampuni imesajiliwa Tanzania na BRELA kwa usajili # 130452,Inalipa kodi kwa kutumia utambulisho (TIN) 132-718-008. Kwa sasa tupo katika hatua za mwishoni kukamilisha usajili wa Hisa za wanajatu katika soko la hisa la Dar es Salaam Yaani (Dar es Salaam stock of exchange ~DSE).
OFISI ZA JATU
Ofisi kuu ipo mkoa wa Dar es salaam, wilaya ya Temeke katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere maarufu kama Sabasaba Maonesho (TANTRADE).
DHIMA KUU YA JATU.
kujenga afya na kutokomeza umaskini kwa kutumia rasilimali watu, kilimo na Viwanda.

HUDUMA ZETU
1. KILIMO
2. VIWANDA
3. MASOKO
4. MIKOPO
5. BIMA YA AFYA
WASILIANA KWA 0763348643 AU 0672285458 KILIMO.
Jatu inamwezesha mkulima kwa kumpa elimu ya shamba, na usimamizi wa shamba kuanzia kuandaa, kupanda, kupalilia hadi kuvuna na kuuza mazao, pia tunatoa mikopo ya kilimo isiyokuwa na Riba kwa mkulima.
Kwa mtu asiye na shamba ila anapesa na anahitaji kuwekeza katika kilimo, Jatu inatafuta maeneo (mashamba) na kuyafanyia utafiti wa kitaalamu na kisheria na ikijiridhisha kwamba ni eneo zuri huwashirikisha wanachama wake ili waweze kuyamiliki mashamba hayo.
Kampuni kwa kutumia wanasheria wake inahakikisha taratibu zote za kisheria katika urasimishaji (umilikishaji) wa ardhi zimefuatwa na Mwanachama anapata hati halali.
Mashamba ambayo Jatu inawashauri watu wake wamiliki ni mashamba makubwa yenye rutuba ambayo yanakubali mazao ambayo kampuni inayahitaji sana katika uzalishaji wake wa bidhaa. Hivyo ina mhakikishia mkulima soko la mazao yake kwani kampuni ina uhakika wa kuyanunua mazao yote kwa wakati na kwa bei halisi ya soko isiyokuwa na madalali. Pia wakulima ambao tayari wanamashamba yao wakijiunga na Jatu kilimo wanapata huduma za usimamizi wa shamba kutoka hatua ya mwanzo hadi mavuno na Masoko.
MASOKO.
kampuni ya Jatu inatumia mfumo wa Masoko ya mtandao (network marketing) kuuza bidhaa zake. Ukijiunga Jatu lazima pia ukubali kununua na kutumia bidhaa zinazozalishwa na jatu. Kila unaponunua unapata sehemu ya faida kwa kila bidhaa uliyonunua (gawio la faida) kila mwezi.
Pia unatakiwa kutengeneza mtandao wa walaji wa bidhaa za Jatu. Kila anaponunua mtu aliye katika mtandao wako kuanzia kizazi cha 1-5 wewe unapata gawio ambalo ni sawa na 40% ya faida yote.
Pia unaweza kuwa wakala wa kampuni na ukafanya kazi ya kutoa semina na kuuza bidhaa zetu katika eneo lako na kampuni itakupa hadi 50% ya faida yote inayopatikana kwa kila bidhaa unayouza. Na pia kama kituo chako Kitaweza kuunganisha mwanachama mpya utapewa kamisheni ya kuendeshea kituo chako.
Pia ukijiunga Jatu na ukawa mjasiliamali unaweza kuuza bidhaa zako kupitia app ya Jatu ambapo ukiwa kokote kule tunakuunganisha na masoko ya kudumu!
VIWANDA.
Kampuni inaanzisha viwanda vidogo karibu na maeneo ya mashamba ambako malighafi zinapatikana na kupitia Viwanda hivi tunanunua mazao ya wakulima ambao ni wanachama wetu na kutengeneza bidhaa ambazo tunaziuza katika mitandao ya wanachama wetu kupitia kwa mawakala wetu ambao hupelekewa bidhaa hadi kituoni kwao.
MIKOPO.
JATU kwa kuwa tuna wanachama wengi na ambao ni wajasaliamali, tumeanzisha Saccos maalumu ambayo ina masharti nafuu ya kukopa kwa wakati na mkopo wa kilimo hauna Riba. Lengo ni kuhakikisha mwanajatu anae fanya kilimo au biashara hakosi mtaji. Ili kuwa mwanajatu saccos kiingilio chake ni tshs.10,000/_ tu.

BIMA YA AFYA.
Kila mwanajatu aliye Jiunga na jatu saccos na amefikisha muda wa miezi Sita ya uanachama (hai) Jatu anapata fursa ya kuunganishwa yeye na familia yake katika mfuko wa BIMA ya afya ya *Resolution* kupitia Jatu. Lakini pia ukiwa mwanachama hai na ukajenga mtandao mzuri wa walaji wa bidhaa za Jatu unapewa BIMA ya afya kama zawadi na kampuni inakua inalipia kila mwaka as long as uko jatu unatumia bidhaa na unajenga mtandao.

BIDHAA ZETU.
kampuni inajikita na bidhaa za chakula na usafi kama vile:
1. Nafaka (Mchele, Dona, na sembe, unga wa lishe na Ngano)
2. Mboga (Maharage, Samaki, Dagaa n.k)
3. Viungo (Mafuta ya alizeti, chai mbadala, Vitunguu, Nyanya, chumvi na sukari n.k
4. Matunda Fresh (Ndizi, Parachichi, nanasi, n.k) na ;
5. Vinywaji ( Maji, Juice mbalimbali na Maziwa)
6. Sabuni, mafuta n.k
Bidhaa hizi baadhi zinazalishwa na Jatu na nyingine zinazalishwa na Mabalozi Yaani wanajatu wajasiliamali wanaouza kupitia Jatu APP.
ANGALIZO:
Hizi Ni jumla ya bidhaa ambazo zinatumika kila siku katika familia zetu. Malengo yetu Ni kwamba ifikapo 2020 mwanajatu apate bidhaa zote za chakula na usafi kupitia app ya Jatu ili anunue na kupata gawio la faida kila mwezi.
"Na hapo tutakuwa tunajenga afya na kutokomeza umaskini "
AINA YA WANACHAMA WA JATU PLC.
1. Mwanachama mteja
2. Mwanachama wa kawaida
3. Mwanachama wakala
4. Mwanachama Balozi

WASILIANA KWA 0763348643 AU 0672285458 MWANACHAMA MTEJA
Huyu Ni mtu yeyote anayejiunga na kampuni kwa lengo la kununua bidhaa za Jatu tu. Huyu Mwanachama analipa kiingilio tu cha 30000 na kujaza fomu ya uanachama. Mwanachama huyu anahaki ya kutengeneza mtandao na akapata malipo ya kila mwezi kutokana na manunuzi yake na ya wanamtandao wake. Hata hivyo mwanachama huyu hataruhusiwa kushiriki miradi mingine ya kampuni kama vile kilimo, saccos Au uwakala. (Kwa sasa unaweza kujiunga bure kupitia Jatu App ambayo inapatikana Playstore~ pakua ujisajili free)

👤 MWANACHAMA. KAWAIDA.
Huyu Ni Mwanachama anayejiunga kwa kujaza hiyo fomu na kuilipia 30000 na baadae akanunua hisa za kampuni kuanzia angalau hisa 50. Hisa moja ya Jatu inauzwa 2500/-. Huyu anapata gawio la kila mwezi kupitia mtandao wake na gawio la kila mwaka kutokana na hisa zake. Huyu mwanachama anaruhusiwa kushiriki miradi mingine ya kampuni isipokuwa uwakala.
👤 MWANACHAMA WAKALA
Huyu ni mwanachama ambaye amejiunga kwa kujaza fomu na amenunua hisa kuanzia 400 ama zaidi, huyu anahaki ya kushiriki fursa zote za JATU ikiwa ni pamoja na kuuza bidhaa za kampuni na kuunganisha wanachama wapya. 

👤 MWANACHAMA BALOZI
Huyu ni mwanachama mbunifu anayeweza kubuni na kuzalisha bidhaa ambazo anazijaza kwenye App ya Jatu na zikauzwa kwa wanachama wa Jatu.

KUJIUNGA JATU PLC.
Kwa wote walioelewa kuhusu JATU na wako tayari kujiunga tafadhali wafike katika ofisi zetu kama ilivyoelekezwa hapo juu, au pakua app ya Jatu Playstore halafu angalia sehemu ya chini kabisa kuna maelekezo ya kutengeneza akaunti yako.
Mara baada ya kusajiliwa na kuwa mwanachama halali wa kampuni, utaruhusiwa kununua hisa kadri ya uwezo wako ambapo kwa mwanachama wa kawaida kiwango cha chini kununua ni hisa 50 na kwa mwanachama atakayehitaji kuwa wakala wa kampuni atatakiwa kununua hisa kuanzia 400. Gharama ya hisa moja ni shilingi elfu mbili na mia tano tu (2500/=).
Kwa mwanachama atakayehitaji kujiunga kwenye kilimo atatakiwa kujaza fomu maalumu ya kilimo ambayo inapatikana ofisini tu kwa gharama ya shilingi elfu ishirini tu (20,000/=) na hivyo kupata fursa ya kushiriki miradi mbalimbali inayohusu kilimo na kusimamiwa na kampuni.

Tovuti: www.jatu.co.tz
App: Playstore ~Jatu
Asante kwa kutuelewa.
Karibu kuwekeza na Jatu PLC.
KUJUA ZAIDI PIGA.
0763348643 au 0672285458
TAZAMA VIDEO HAPA:

No comments

Powered by Blogger.